MWANRI AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA KATA NA MATAWI, JIMBO LA ILALA

MWANRI AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA KATA NA MATAWI, JIMBO LA ILALA

Naibu Katibu Mkuu Bara ndugu Aggrey Mwanri (MCC) leo tarehe 13 Oktoba 2026, Jimbo la Ilala amefungua Semina ya mafunzo kwa viongozi wa Kata na matawi katika Jimbo la Ilala.

Mafunzo ni muendelezo wa kuwajengea uwezo viongozi wa CCM.katika itikadi ya Chama, Maadili na kuongeza wanachama wa CCM.

Aidha ndugu Mwanri amesisitiza Umuhimu wa viongozi kuzingatia maadili katika maisha yao ya kila siku kwani wamebeba taswira ya CCM kila mahali lakini pia amesisitiza viongozi kuwa waadilifu wakati wote.

Katika hatua nyingine, ndugu Mwanri amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika Jimbo la Ilala na Mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla, lakini pia amempongeza Mhe. Azan Zungu, Mbunge wa Jimbo la Ilala na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutimiza wajibu wake ipasavyo katika Jimbo lake licha ya kuwa na majukumu mengi.

Hata hivyo, Mhe. Zungu nae alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Mkutano wa 153 wa Mabunge ya Dunia ufanyike Tanzania na amemshukuru kwa kutenga fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi katika Jimbo la Ilala

Kwa Upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ndugu Stanley Mkandawire (MNEC) amesisitiza Umuhimu wa mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa na kuwaomba viongozi wakawe mabalozi wazuri kwa jamii baada ya kupata mafunzo 

Pia, ndugu Juma Simba Gadafy ambae ni Mjumbe wa NEC Taifa anaewakilisha Mkoa wa Dar es salaam alimpongeza Mhe. Zungu kwa kuwa na utaratbu mzuri wa uwasilishaji wa utekelezaji wa ilani kwa waliompa dhamana.

Mwisho, Mhe. Azan Zungu aliwashukuru viongozi hao kwa kufika na kuwa na utayari na morali ya kujifunza hiyo inaonesha mshikamano ndani ya CCM.

 Mbunge wa Jimbo la Ilala na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Azan Zungu, akizunguza katika semina hiyo.
Taswira ya semina hiyo.
Semina ikiendelea

 

Post a Comment

0 Comments