KAWAIDA APOKELEWA MKOA WA RUKWA

KAWAIDA APOKELEWA MKOA WA RUKWA

Vijana wa Itifaki wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wakimvika Skafu Mwenyekiti wa Umoja huo, Mohammed Ali Kawaida (MCC) Oktoba 13, 2026, wakati akipokelewa  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa,

...............

Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Ali Kawaida (MCC) leo Oktoba 13, 2026, amepokelewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa, kuelekea kushiriki kama Mgeni Rasmi katika Kongamano la Wiki ya UVCCM kitaifa 2026 mkoani humo.

Baada ya mapokezi, Mwenyekiti amefanya kikao cha ndani na viongozi wa Chama na Jumuiya kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za UVCCM na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya vijana.

Kaulimbiu: Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana.

Mapokezi ya kiongozi huyo yakifanyika mkoani Rukwa.
 

Post a Comment

0 Comments