Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali pamoja na mabadiliko ya Walezi wa Mikoa, katika kikao chake maalum kilichofanyika leo, Oktoba 11, 2026, Kizimkazi, Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Laban Kihongosi, Kamati Kuu imemteua Dkt. Nettho Ndijina Ndilito kuwa Mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma.
Katika uteuzi mwingine, Kamati Kuu imemteua Faris Buruhani kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambapo kabla ya uteuzi huo, Faris alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera.
Aidha, Kamati Kuu imefanya mabadiliko madogo ya Walezi wa Mikoa, ambapo Deogratius John Ndejembi ameteuliwa kuwa Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, huku Kenani Laban Kihongosi akiteuliwa kuwa Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma.









0 Comments