CCM MANYARA YAENDELEA NA MAFUNZO YA MAKADA, USAJILI WA WANACHAMA WAPYA

CCM MANYARA YAENDELEA NA MAFUNZO YA MAKADA, USAJILI WA WANACHAMA WAPYA

Mafunzo ya Ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Maandalizi ya Makada wa  chama hicho  Mkoa wa Manyara yakiendelea kwa kasi kubwa Oktoba 13, 2026.

.....................................

Na Mwandishi Wetu, Manyara

Mafunzo ya Ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maandalizi ya Makada wa chama hicho Mkoa wa Manyara yameendelea kupamba moto, huku yakiingia siku ya tano tangu kuanza kwake.

Katika kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Maandalizi ya Makada, Mwalimu Yusuph Ally Rajab, amefanya ziara katika baadhi ya kata zinazoshiriki mafunzo hayo kwa lengo la kujionea namna yanavyotekelezwa.

Katika ziara hiyo, Mwalimu Rajab ametembelea Kata ya Magara, iliyopo Wilaya ya Babati Vijijini; Kata ya Maisaka, Wilaya ya Babati Mjini; pamoja na Kata ya Hirbadaw, iliyopo Wilaya ya Hanang.

Mafunzo hayo yanaenda sambamba na shughuli za kusajili wanachama wapya wa CCM pamoja na kuhamasisha ulipaji wa ada za uanachama.

Shughuli hizo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Ujenzi wa Chama na Maandalizi ya Makada, ambayo inaendelea katika kata mbalimbali za Mkoa wa Manyara na maeneo mengine nchini.

Mafunzo hayo yanalenga kuendeleza maandalizi ya makada na kuimarisha shughuli za chama kupitia programu inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali.

Taswira ya mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa darasani.
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiwa yamepamba moto.

Kwa habari mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi (CCM piga  namba 0754362990
 

Post a Comment

0 Comments