.......................................
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Pwani Oktoba 17, 2026, huku wananchi wa mkoa huo wakitarajiwa kumpokea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, Kihongosi ataanza ziara hiyo wilayani Rufiji Oktoba 17, 2026, kabla ya kuelekea wilayani Mkuranga Oktoba 18, mwaka huu.
Ziara za kikazi anazofanya Kihongosi katika mikoa mbalimbali nchini zinalenga kukagua uhai wa chama na juhudi za kukiimarisha, kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM kupitia miradi ya maendeleo, pamoja na kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero zinazowakabili wananchi.
......................................
Habari hii imeandikwa na Dotto Mwaibale Simu namba 0754362990









0 Comments