MKURUGENZI KAMPUNI YA GBP KIONGOZI MWENYE UPENDO ANAYEGUSWA NA MAISHA YA WENGINE

MKURUGENZI KAMPUNI YA GBP KIONGOZI MWENYE UPENDO ANAYEGUSWA NA MAISHA YA WENGINE

 Awasili Kizimkazi kumfariji Rais Samia kwa kufiwa na Mume wake.


 Mkurugenzi Mkuu Wa Kampuni Ya GBP Badar Sood akimfariji Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 08, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, Septemba 07, 2026,

................................................ 

Na Dotto Mwaibale, Tanga

UPENDO ni hali ya moyo wa mtu kuwa na hisia kali ya  kujali, kuhurumia kuwa na uchungu dhidi ya mtu mwingine bila ya kinyongo.

Ni sifa ya thamani inayohusisha ustahimilivu  na kutafuta mema kwa wengine kama vitabu vitakatifu vya dini zote kwa Waislaamu Qur-an na Biblia kwa Wakristo vinavyoeleza upendo kama amri kuu, ikimaanisha ni msingi wa maisha ya kiroho.

Mkurugenzi Mkuu Wa Kampuni Ya GBP ya Jijini Tanga, Badar Sood ni kiongozi   mwenye upendo ambaye anagusa maisha ya watu mbalimbali.

Wananchi wa Mkoa wa Tanga na maeneo mengine ya nchi wana ujua ubinadamu wake. 

Badar Sood   wakati wote amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali ya maendeleo, furaha na huzuni.

Jambo hilo limekuwa likimuweka jirani zaidi na wananchi na kufanya apendwe. 

kutokana na hulka yake ya kuwa na wananchi karibu amekuwa akiweka kipaumbele hasa wanapokuwa na changamoto mbalimbali zikiwepo za ugonjwa.

Kiongozi huyu amekuwa akionesha upendo wake kwa watu wote bila ubaguzi.

Katika kudhihirisha upendo alionao Septemba 8, 2026, Badar Sood alifika Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar wakati akipatiwa matibabu, Septemba 07, 2026.

Jambo hilo siyo dogo kwani ni la kiimani zaidi na dini zote zimekuwa likihimiza.

 Maisha ya Badar Sood yamekuwa kielelezo kwa wana Tanga na Taifa kwani ni mtu mwenye hofu ya Mungu na asiye jikweza.

.......................

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale Simu namba 0754362990.

Post a Comment

0 Comments