WANANCHI WA
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida wamempongeza Dk. Samia Suluhu
Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya
ambayo imekuwa mkombozi wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofanya ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo Agosti
12, 2026, Janeth Khalid Mkazi wa Mlandizi Itigi alisema wanakila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais kwa
kazi kubwa aliyoifanya siyo kwa Itigi pekee bali kwa nchi nzima.
“Tunatoa shukrani zetu kwa Rais Samia kwa kutujengea hospitali hii hasa kwa sisi wanawake ambayo gharama zake ni ndogo tofauti na Hospitali ya Rufaa ya St. Gasper,” alisema Khalid.
Khalid
alisema katika hospitali hiyo huduma zote muhimu wanazipata ikiwemo ya upasuaji
jambo ambalo limewapunguzia gharama ya kusafiri kwenda hospitali nyingine kubwa
zilizopo mkoani Singida na Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Mkazi wa
Mlowa mjini Itigi Getrude Masanja aliwapongeza wauguzi, madaktari na watumishi
wengine wa hospitali hiyo chini ya usimamizi wa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,
Dk. Emmanuel Mallange kwa huduma nzuri
wanayoitoa.
“Dada yangu alipokuwa amelazwa katika hospitali hiyo alikuwa akihudumiwa vizuri na siyo pekee bali na wagonjwa wengine hakika sifa na utukufu apewe Mwenyezi Mungu kwa kazi wanayoifanya,” alisema Masanja.
Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Itigi, Dk. Emmanuel Mallange alisema uboreshaji wa hospitali hiyo umeleta matokea makubwa ya kuwahudmia
wananchi kwa wingi ambazo walikuwa hawazipati hapo awali.
“ Hii ni kama Hospitali ya Rufaa ndani ya Halmashauri yetu ambapo wagonjwa wanatoka kwenye Zahanati na kuja ngazi ya wilaya,” alisema Dk. Mallange.
Alisema
tangu waanze kuboresha hospitali hiyo wamejenga majengo saba ambayo yote
yanatumika kwa ajili ya kutoa huduma.
Dk. Mallange
aliyataja majengo hayo kuwa ni ya
wagonjwa wa nje, mionzi, kufuria, dawa, wazazi pamoja na upasuaji.
Aliongeza
kuwa kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ayubu Kambi
katika bajeti ya mwaka huu Serikali imewapa fedha ambapo inatarajia kujenga jengo
la upasuaji, watoto, wodi ya wakina mama pamoja na wodi ya wanaume.
“Naamini kupitia Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wataendelea kupata huduma nzuri,” alisema Dk. Mallange.
Dk. Mallange
ametoa rai kwa wananchi wote wa Halmashauri hiyo kufika katika hospitali hiyo
watapata huduma nzuri na kueleza kuwa mpaka hivi sasa wanawake 26 ambao
walishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida waliwafanyia upasuaji na wanaendelea
vizuri pamoja na watoto wao.Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Itigi, Dk. Shabani Mahenge akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipo tembelea chumba cha huduma ya kinywa na meno.
Waandishi wa habari wakitembelea jengo la mionzi katika Hospitali hiyo.
Muonekano wa chumba cha Maabara katika Hospitali hiyo.
Muonekano wa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo.








0 Comments