Dk.Stellaa Joel aakionesha cheti baada ya kutunukiwa. Wengine ni viongozi wa Christian Ministerial Traning Universty na Wageni waalikwa.
.....................................
WANAMUZIKI Jijini
Arusha wametunga wimbo maalumu kwa ajili ya kumpongeza Katibu Mkuu na Mwanzilishi
wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Stella Joel baada ya kutunukiwa tuzo mbili ya kwanza ni ya udaktari aliyopewa na Christian Ministerial Traning Universty na Umoja wa Wanamuzi wa Zambia kupitia Serikali yao kutokana na
mchango wake mkubwa kwenye tasnia hiyo.
Wimbo huo utazinduliwa katika hafla itakayofanyika Jijini Dar es Salaam Agosti 21,2026 na kuhudhuriwa na wanamuziki mbalimbali.
Mwanamuziki Benjamin
Nzogu mmoja wa watunzi wa wimbo huo alisema Stella amekuwa na mchango mkubwa
amewainua sana katika kazi ya muziki.
“Tukizungumza kati ya tuliotunga wimbo huo binafsi Dk. Stella ni mtu ambaye ametuinua sana, anajali kazi zetu na kutupa fursa mbalimbali na kutuunganisha na wadau ambao wamekuwa wakitusaidia na baada ya kutunukiwa tuzo hiyo tukaona hatuna cha kumpa zaidi ya kumtungia wimbo,” alisema Nzogu.
Mwanamuziki
mwingine aliyeshiriki katika wimbo Rachel Mmassy amesema kwa hakika Stella
amekuwa na mchango mkubwa kwa wanamuziki hapa nchini hasa chipukizi.
“ Dk.Stella ni dada ambaye anajituma sana na kuwa na sapoti kwetu kwa kutuunganisha na makundi mengine ya watu kwa lengo la kupata ushauri na hata rasilimali fedha,” alisema Mmassy.
Alisema Tuzo
aliyotunukiwa Dk. Stella ni ya muhimu sana kwani inaonesha wanawake nao wanaweza
kufanya chochote chema wanapo thubutu kufanya na aamewaheshimisha sana.
Wanamuziki
walioshiriki wimbo huo ni Benjamin Nzogu, Japhet Idrisa, Chance Lipomrushi,
Rachael Mmassy, Joel Mmassy, Rose Machibaya, Salome Ellyn a David Mboya.
Dk.Stella Joel
tuzo hiyo aliyotunukiwa ni ya tatu ambapo ya kwanza alitunukiwa na Chama cha Hati Miliki Tanzania (COSOTA) mnamo
Aprili 2022.
Tuzo hiyo
ilitolewa kutambua mchango wake mkubwa katika kuhamasisha maendeleo ya muziki
na kuhakikisha wanamuziki wanasajiliwa ili kutambuliwa na serikali.
Tuzo yake ya pili alitunukiwa na Kampuni ya Phide Intertermet and Tours yenye makao yake makuu jijini Arusha inayojishughulisha na masuala ya utalii hapa nchini.
Dk. Stella Joel akionesha cheti baada ya kutunukiwa.
Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.











0 Comments