Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigezi Chini, Musa Singano, akizungumzia kuhusu mtanange huo..
..............................................
Na Mwandishi Wetu.TIMU 16 zinatarajia kuwania ubingwa wa Singano Cup katika mashindano ya soka yaliyopangwa kuanza Jumamosi wiki hii, Kigezi Chini, Buyuni, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigezi Chini, Musa Singano, timu itakayotwaa ubingwa itazawadiwa ng'ombe 'mnyama'.
Katika mashindano hayo, ambayo yatazinduliwa Jumamosi wiki hii, mshindi wa pili ataondoka na Mbuzi.
Akizungumza Agosti 17, mwaka huu, ofisini kwake, Singano alisema kuwa mashindano hayo yameanzishwa kwa lengo la kuibua vipaji chipukuzi vya soka na kuviendeleza kwa faida ya baadaye kwa timu za Taifa.
Singano alisema kuwa pamoja na kuibua vipaji vya soka, pia mashindano hayo yanalengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan za kuendeleza michezo nchini.
"Tunajumuika pamoja kumuunga mkono Rais Samia katika kuendeleza michezo ikizingatia mwakani tunakuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Afrika (AFCON)," alisema Singano. Alisema kuwa kauli mbiu katika mashindano hayo ni AFCON na Mama Samia.
Mwenyekiti huyo, alisema kuwa michezo inagusa maisha ya watu wengi na ni ajira kwa vijana,
Pia, alisema kuwa mashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo timu 16 zitapangwa katika makundi manne.
Katika hatua hiyo, kila kundi litatoa timu mbili ambazo zitaingia robo fainali, baadaye nusu fainali na fainali.









0 Comments