PROFESA NOMBO ATEMBELEA BANDA LA TEA, MAONESHO YA ELIMU, UJUZI, AFURAHISHWA NA WANAFUNZI WA AMALI

PROFESA NOMBO ATEMBELEA BANDA LA TEA, MAONESHO YA ELIMU, UJUZI, AFURAHISHWA NA WANAFUNZI WA AMALI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo (kulia) akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA), Mwanahamis Chambega, alipotembelea Banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika Maonesho  ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga, Agosti 2026.

...........................

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo ametembelea Banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika Maonesho  ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga, Agosti 2026.

Katika banda hilo Profesa Nombo amefurahishwa na Wanafunzi wa Amali kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe kwa namna walivyokuwa wamepika vitafunwa (maandazi) baada ya kufundishwa na walimu wao wanao hudhuria Maonesho hayo.

“Hongereni kwa mapishi mazuri ya maandazi  mliyoyaandaa,” alisema Profesa Nombo.

Mwanafunzi Najma Baraka ambaye anashiriki Maonesho hayo amesema mafunzo ya Amali anayapenda na anataka kuwa mpishi wa viwango vya juu wa kutengeneza keki, maandazi, karanga za mayai, Bisi (Rock bur, Pop corn) na vingine vingi vinavyofanana na hivyo.

Mwanafunzi Ntuli Danken amesema mafunzo ya Amali ni muhimu kwa wanafunzi kwani yana waandaa kujitegemea kabla na  baada ya masomo yao. 

Mwanafunzi wa Amali kutoka Shule ya Wasichana ya Korogwe, Najma Baraka akimkabidhi zawadi ya Vitafunwa alivyo viandaa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo katika maonesho hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo, akimuangalia Mwanafunzi Najima Baraka alivyokuwa akiandaa vitafunwa katika maonesho hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo, akiwaelekeza jambo Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ambao wameshiriki maonesho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA), Mwanahamis Chambega.
Wanafunzi wa Amali kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe, Ntuli Danken na Najma Baraka wakitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo (hayupo pichani), alipotembelea Banda la TEA katika maonesho hayo. Kulia ni Mwalimu wa Mafunzo ya Amali (mapishi), kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe, Catherine Machugu. 
Wafanyakazi wa TEA wakiwa kwenye banda lao wakimsubiri Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo kabla ya kutembelea kwenye maonesho hayo. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa TEA, Eliafile Solla, Afisa Miradi ya Elimu Kabula Jullu, Mtumishi wa TEA, Afisa Miradi ya Elimu, Joyce Minja na Mwalimu wa Mafunzo ya Amali, Catherine Machugu.

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990

Post a Comment

0 Comments