Mhe. Ally Minja Diwani wa Kata ya Itigi Mjini, ambaye aliandika andiko la kuanzisha Mfuko wa Elimu, akizungumza katika baraza la madiwani Agosti 12, 2026 kuhusu faida ya mfuko huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Ipande, Kedmon Mpondo.
.........................
MFUKO wa Kusaidia Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida unatarajia kuanzishwa baada ya Diwani wa Kata ya Itigi Mjini Ally Minja kuandika andiko na kulipeleka kwa madiwani na kupokelewa.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani lililoketi Agosti 12, 2026 kwa lengo la kupokea, kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo (ikiwemo miundombinu, afya, elimu na maji) kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Itigi, Mhe. William Lupaa alisema wazo hilo limepokelewa kwa mikono miwili na Madiwani.
“ Wazo hili kupitia andiko la Mhe. Ally Minja Diwani wa Kata ya Itigi Mjini ni zuri na tumelipokea kwa mikono miwili lakini tumelipeleka kwenye Kamati ya Elimu na Afya ili likajadiliwe na kuona hatua nyingine zitakazo fuata,” alisema Lupaa.
Akizungumzia manufaa ya mfuko huo Mhe Minja alisema suluhisho la pamoja aliloliona hadi kufikia tafakari hiyo ni kuiomba Halmashari ya Wilaya ya Itigi kuanzisha Mfuko wa Elimu kwa ajili ya kukusanya rasilimali fedha kutoka maeneo mbalimbali.
“Fedha zitakazopatikana zitawasaidia watoto na kizazi chetu kiweze kupata elimu,” alisema Minja.
Minja alisema ikumbukwe kwamba kipaumbele cha elimu ni kikubwa kuliko vingine vyote na ndiyo urithi mkubwa ambao ni miongoni na ule watakao achiwa.
Akielzea namna ya kupata fedha hizo ni pamoja na kuanzisha uhamasishaji wa upatikanaji wa fedha ya kusomesha watoto na kutafuta njia bora nyingine za kupata fedha hizo.
Akitolea mfano mwingine alisema “Agosti 11 katika halmashauri hiyo ulifanyika mnada ambao waliuza kilo milioni 2.5 za dengu ambapo kama wangewaomba wakulima kupitia vyama vyao angalau shilingi 10 tu kwenye kila kilo ambayo inaweza kuonekana haina kazi lakini kwa mnada huo uliofanyika wangeweza kupata shilingi milioni 25.
“Kwa mnada wa jana tu tungeweza kupata kiasi hicho cha fedha ambazo zingeingia kwenye mfuko huo na mpaka minada mingine ije imalize msimu ingekuwa tumepata shilingi ngapi,” alihoji Minja.
Aidha, Minja alisema hiyo ni kwa zao la ndengu je wakienda kwenye zao la pamba ambalo linauzwa kwa ushirika ambayo inalimwa kwenye vijiji vya Kitaraka, Lyandole na kata nyinge hapo hawajaenda kwenye zao la tumbaku na kupata michango kutoka taasisi mbalimbali na Asasi nyingine kuchangia elimu.
Minja aliongeza kuwa hilo wazo linaweza kuonekana la kawaida kwa sasa kwa sababu baadhi ya watu wamezoea kuweka ubinafsi mbele lakini shida ya mtoto kukosa fedha za kumuendeleza kusoma linaikumba kila nyumba.
Alisema jambo hilo ni kama ilivyo kwa maradhi na hakuna ukoo ambao haujawahi kukumbwa na changamoto ya mtoto kushindwa kuendelea na masomo kwa kukosa rasilimali fedha hivyo halmashauri hiyo ikianzisha mfuko huo itaweza kusaidia watoto kwa mamia kuweza kuendelea na masomo ambao utakuwa msaada mkubwa sana.
Makaamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Itigi, William Lupaa, akiongoza baraza hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ayubu Kambi na Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala, Charles Magesa.Madiwani wakiwa kwenye baraza hilo.
Waratibu wa vikao wa Halmashauri hiyo (CC), wakiwa kazini. Kushoto ni Juliana Jephata Kaaya na Makandaiga Chacha Magabe wakishiriki baraza hilo.








0 Comments