CHINA YAVUTIWA UWEZO WA WANAFUNZI MKONDO WA AMALI MKOANI TANGA

CHINA YAVUTIWA UWEZO WA WANAFUNZI MKONDO WA AMALI MKOANI TANGA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi Jackline Habibu Ndee (kushoto), ambaye anajifunza masomo ya Amali alipotembelea banda la mkondo wa Amali kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga Agosti 18, 2026.
....................................

Balozi wa Tanzania nchini China, Dkt. Suleiman Haji Suleiman, ameeleza kuwa makampuni kutoka nchini China yamevutiwa na uwezo mkubwa na kazi nzuri zilizofanywa na wanafunzi wa mkondo wa Amali.

Hayo aliyasema Agosti 18, 2026 wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea Viwanja vya Shule ya Sekondari yaa Usagara Jijini Tanga ambapo Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda alikuwa mgeni rasmi.

Balozi Suleiman Haji Suleiman alisema  kutokana na umahiri huo, makampuni hayo yako tayari kutoa ufadhili wa masomo na mafunzo kwa wanafunzi hao hapa Tanzania na nchini China, pamoja na kuwapa ajira ya moja kwa moja baada ya masomo.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Carolina Nombo amesema Tanzania imejipanga kuishangaza dunia katika mashindano ya ujuzi kwa vijana baada ya kuanza kuwaandaa kwa kiwango cha kimataifa washindi wa nafasi za juu. 

Prof. Nombo amefafanua kuwa Tanzania sasa ni mwanachama wa Shirika la Mashindano ya Ujuzi Duniani - WorldSkills Competition, hivyo imeanza kushiriki mashindano ya kimataifa kufuatia maelekezo ya viongozi wa ngazi za juu.

"Kwa hiyo Tanzania tumeanza na tutahakikisha tunawaandaa vijana wetu kuonesha ujuzi wao wa kiwango cha juu ili dunia nayo itambue kuwa tuna vijana mahiri ambao wanaweza kushindana kwenye majukwaa ya kimataifa," amesema.

Balozi wa Tanzania nchini China, Dk. Suleiman Haji Suleiman akizungumza wakati wa kutembelea banda ya mkondo wa Amali kabla ya kuzinduliwa kwa Maonesho hayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Carolina Nombo akizungumza.

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.

 

Post a Comment

0 Comments