CCM YAIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI KWA MAENDELEO

CCM YAIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI KWA MAENDELEO

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni na Itigi, Maimuna Likunguni akitoa salamu za chama kwenye kikao cha Baraza la Madiwani lililoketi Agosti 12, 2026 wilayani Itigi mkoani Singida.

............................

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwa kutekeleza vizuri ilani ya chama hicho kwenye miradi ya maendeleo.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni na Itigi, Maimuna Likunguni kwenye kikao cha Baraza la Madiwani lililoketi Agosti 12, 2026 kwa lengo la kupokea, kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo (ikiwemo miundombinu, afya, elimu na maji) kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

“Mhe. Mwenyekiti awali ya yote nitumie nafasi hii kukupongeza wewe binafsi kwa namna unavyo unavyosimamia Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa kushirikiana na madiwani wote wa halmashaauri hii,” alisema Likunguni.

Aidha, Likunguni alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwasimamia vizuri wakuu wa idara na  vitengo mbalimbali na kuifanya halmashauri hiyo kusonga mbele kimaendeleo.

“Mhe. Mwenyekiti niendelee kukupongeza kwa halmashauri yetu kuongoza kukusanya mapato kwa miaka mitatu mfululizo ni jambo la kujivunia sana,” alisema Likunguni.

Alisema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa na madiwani, ofisi ya Mkurugenzi na timu ya Wataalamu.

Likunguni alisema suala la ukusanyaji mapato ni kubwa na kuwa kwa mtu mmoja mmoja peke yake haiwezekani.

Aliongeza kuwa suala hilo kwa mtu mmoja haiwezekani kwa kuwa fedha hizo  zinakusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya biashara na kwenye mazao na maeneo mengine yanayofanana na hayo.

“Kwa hali hiyo mtu kutoa fedha yake bila kumshawishi vizuri siyo jambo dogo hivyo kutokana na ushirikiano mliokuwa nao sisi kama Chama Cha Mapinduzi tunaridhishwa sana niwaombe muendelee kushikamana na kuwa na ushirikiano ili halmashauri yetu iendelee kutambulika zaidi kimkoa na Taifa kwa ujuma,” alisema Likunguni.
Madiwani wakiwa kwenye baraza hilo.Taswira ya baraza hilo.

Waratibu wa vikao wa Halmashauri hiyo (CC), wakiwa kazini. Kushoto ni Juliana  Jephata Kaaya na Makandaiga Chacha Magabe wakishiriki baraza hilo.

Habari hii imeandaliwa na Msimamizi Mkuu wa Uenezi CCM Blog, Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.
 

Post a Comment

0 Comments