ZAVALA WASOGEZEWA HUDUMA YA AFYA, RAIS SAMIA AMWAGIWA SIFA

ZAVALA WASOGEZEWA HUDUMA YA AFYA, RAIS SAMIA AMWAGIWA SIFA

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Zavala uliopo Kata ya Buyuni Ilala Jijini Dar es Salaam Faridu Sadiki akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

.............................................

Na Mwandishi Wetu.  

WANANCHI wa Zavala, Kata ya Buyuni, Ilala, jijini Dar es Salaam, wamesogezewa huduma ya afya karibu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati yao.

Zahanati hiyo, ambayo ya kisasa imekamilika kutokana na mipango mizuri ya viongozi wa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.  

 Akizungumza juzi, wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu iliyojengwa katika mtaa wa Zavala, mwenyekiti wake, Faridu Sadiki alisema kuwa mafanikio hayo ni ukombozi kwa wananchi wake, ambao walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.  

Sadiki alisema kuwa katika mtaa wake wamefanikiwa kupata miradi miwili ya ujenzi wa daraja na Zahanati. 

Alisema miradi hiyo imejengwa kwa fedha za serikali na kituo cha polisi kwa nguvu ya wananchi.                  

Mwenyekiti huyo, alimpongeza Rais Samia, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpongolo kutokana na jinsi wanavyotekeleza ipasavyo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).  

Sadiki alisema kuwa baada ya kufanikisha ujenzi wa Zahanati, kwa sasa wananchi wa Zavala wanapata huduma ya afya karibu tofauti na awali.

 "Zahanati yenu imefunguliwa rasmi Aprili 14, mwaka huu, niwaombe wananchi wangu kwenda kupata huduma pale Zahanati ina madaktari na vifaa tiba vyote," alisema Sadiki.  

Pia alisema kuwa  wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Mtaa wa Zavala na Mbondole ambalo limejengwa kwa fedha za serikali.   

Pamoja na miradi hiyo, serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara  kwa kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilometa nne. 


Muonekano waa majengo ya Zahanati ya Zavala baada ya kukamilika.
 

Post a Comment

0 Comments