𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗠𝗛𝗘. 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗦𝗨𝗟𝗨𝗛𝗨 𝗛𝗔𝗦𝗦𝗔𝗡 𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜 𝗝𝗜𝗝𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗢𝗦𝗖𝗢𝗪 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗡𝗜 𝗨𝗥𝗨𝗦𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜 𝗬𝗔 𝗭𝗜𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔.

𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗠𝗛𝗘. 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗦𝗨𝗟𝗨𝗛𝗨 𝗛𝗔𝗦𝗦𝗔𝗡 𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜 𝗝𝗜𝗝𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗢𝗦𝗖𝗢𝗪 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗡𝗜 𝗨𝗥𝗨𝗦𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜 𝗬𝗔 𝗭𝗜𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, uliopo Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa, nchini Urusi tarehe 02 Juni, 2026. Ziara hii ina lenga kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi Mhe. Maxim Reshetnikov wakati Gwaride la Heshima likipita mbele katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, Jijini Moscow nchini Urusi tarehe 02 Juni, 2026.

Post a Comment

0 Comments