KIBAGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI

KIBAGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI

              Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibaga, Kata ya Kinyerezi, Ilala,  Dar es Salaam, Revina Lyakulwa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

..........................

Na Mwandishi Wetu.         

 MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Kibaga, Kata ya Kinyerezi, Ilala,  Dar es Salaam, Revina Lyakulwa, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuwatengenezea na kuboresha miundo mbinu ya maji katika kata hiyo. 

Akizungumza juzi ofisini kwake, Revina alisema kuwa alipoingia madarakani Novemba 28, 2024, alikuta hali ya upatikanaji wa maji ni wa shida.

Revina alisema kuwa kwa muda mfupi baadaye wananchi wa Kibaga walianza  kupata maji angalau kwa wiki mara mbili baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji la Bangulo. 

Mwenyekiti huyo, alisema kuwa mafanikio ya watu wake kupata huduma ya maji yanatokana na jitihada za Rais Samia na diwani wa Kata ya Kinyerezi ambaye ni Naibu Meya wa Ilala, John Lyioba kuendelea kuwaletea wananchi wao maendeleo.

"Nampongeza Rais Samia amebeba dhamira ya kweli ya kusimamia kwa uweledi sekta nyingine kama elimu na afya," alisema Revina. 

Alisema kuwa kwa sasa wanatarajia kuboresha zaidi miundo mbinu ya maji kwa kuchimba kisima kwa kushirikiana na DAWASa ili waweze kusambaza maji mtaa mzima.

Revina alisema kuwa pamoja na kutengeneza miundo mbinu ya maji, lakini kwa kipindi alichokalia kiti hicho, ameweza kuchonga na kuweka kifusi katika barabara za mitaa kwa kushirikiana na diwani wake.                                  

Pia alisema kuwa, aliweza kuboresha ofisi ya mtaa huo, kwa kuweka umeme, milango, madirisha, taires na vyoo.

Katika hatua nyingine, Revina ameiomba Serikali kupitia Halmashauri ya Ilala kutenga bajeti ya fedha ili  waweze kujengewa Zahanati. 

Revina alisema kuwa  eneo la kujenga Zahanati hiyo wanalo, lakini hawana fedha, kwani wananchi wake wanasumbuka kufuata huduma ya afya umbali mrefu.  

Akizungumzia upande wa elimu, mwenyekiti huyo, alisema kuwa mtaa wake una shule mbili, moja ya msingi na nyingine ya sekondari.

Alisema kuwa Shule ya Msingi ya Kibaga ina upungufu wa madarasa na madawati,  kwani wanafunzi ni wengi wanaosoma shuleni hapo. 

Post a Comment

0 Comments