WASSIRA: CCM NDIYO CHAMA PEKEE KINACHOJALI MASLAHI YA TAIFA

WASSIRA: CCM NDIYO CHAMA PEKEE KINACHOJALI MASLAHI YA TAIFA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Tanzania Bara Cde Steven Masato Wassira, akizungumza na Wanachama wa Wilaya za Buhigwe na Kasulu mkoani Kigoma katika ziara ya kawaida ya kuimarisha Chama Mei 16, 2026.

.....................................

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Tanzania Bara Cde Steven Wassira amesema CCM ndio Chama pekee kinachojali maslahi ya Taifa na kuwapigania wananchi kimaendeleo.

Wassira ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama katika Wilaya za Buhigwe na Kasulu mkoani Kigoma katika ziara ya kawaida ya kuimarisha Chama.

Amesema Chama kina malengo na madhumuni ambayo kila mwanachama na kiongozi anatakiwa afahamu na kuyaishi ili kujenga uzalendo wa Taifa.

Kutoakana na hali hiyo amewaagiza matibu wa siasa, uenezi na mafunzo wa  CCM kuanzia Tawi hadi Mkoa kutoa mafunzo kwa wanachama ili wakijue Chama Chao na malengo yake katika Taifa na kuwatumikia wananchi.

Amesema pamoja na lengo kuu la kushinda uchaguzi CCM ina wajibu wa kulinda na kudumisha uhuru wa nchi, kuhimiza ujenzi wa ujamaa na kujitegemea kwa mujibu wa azimio la Arusha, kusimamia utekelezaji wa siasa na kuona kila mtu anapata haki katika shughuli za maisha yake.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara anaendelea na ziara yake ambapo atakutana na Halmashauri kuu ya CCM Mkoa na kuhutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kigoma, Jamal Tamim, akizungumza.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kigoma, Jamal Tamim akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Tanzania Bara Cde Steven Wassira.Kikao kikiendelea

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Tanzania Bara Cde Steven Wassira. akisalimiana na viongozi mbaalimbali wa chama hicho.
Kikao kikiendelea.
Mkutano ukiendelea.
 

Post a Comment

0 Comments