Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo akiongoza kikao kazi cha Makatibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Mkoa huo kilichoketi Mei 20, 2026 kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha uhai wa chama.
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kigoma Christopher Pallangyo akifungua kikaao kazi kazi hicho alisema chama hicho kimeanza hatua ya kujitathmini ili kwenda na wakati na kukidhi mahitaji ya jamii.
Kikao kazi hicho ambacho kimeandaliwa na Idara ya Uenezi Mkoa na kimepanga mipango mbalimbali, kimehudhuriwa na Makatibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo kutoka wilaya za Kakonko Cde. Nelso Kisinga, Kasulu Cde. Joel Madelele, Buhigwe Cde. Ngatura Ramadhan, Kigoma vijijini Cde. Kasongo Abdul Cheko, Kigoma mjini Cde. Haruna Kambiro na wilaya ya Uvinza Cde. Mohammed Ruhura.
Katibu wa siasa, uenezi na mafunzo CCM Mkoa wa kigoma Deogratius Nsokolo amesema kikao hicho ni mwanzo wa mkakati mkubwa wa kuimarisha Chama kuanzia ngazi ya shina.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Christopher Pallangyo akifungua kikao hicho.Kikao kikiendelea
Kikao kikiendelea

Picha ya pamoja
Picha ya pamoja












0 Comments