Haya hapa majukumu yake
Mhe. Angela Charles Kizigha Mshauri wa Rais Masuala ya Jamii.
..........................
MAENDELEO ya
jamii ni jambo ambalo husaidia kuwawezesha mtu mmoja mmoja au vikundi vya kijamii kuleta mabadiliko katika jamii zao.
Ili kufikisha maendeleo hayo kwa jamii inatakiwa kupewa maarifa, ujuzi na kuunda vikundi vitakavyokuwa na
kazi na ajenda maalumu.
Maendeleo ya Jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hutafsiriwa kama Mchakato wa wanajamii kukusanyika pamoja kwa ajili ya kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili.
Kutokana na unyeti na ukubwa wa masuala ya maendeleo ya kijamii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Angela Charles Kizigha kuwa mshauri wake wa masuala ya kijamii.
Kuaminiwa
kwa Kizigha na Rais kwenye nafasi hiyo kunatokana na uwezo wake na anakwenda
kumsaidia katika kubuni na kusimamia mikakati ya kijamii yenye tija kwa
wananchi, sambamba na kushauri juu ya changamoto zinazoikabili jamii.
Aprili 20,
2026, Mhe. Kizigha aliteuliwa na Rais Samia kuwa Mbunge na kufuatia uapisho
wake uliofanywa na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu.
Kizigha ana uzoefu na mchango mkubwa wa kulitumikia Taifa kuanzia kwenye
chama ambapo ameshika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa
wa Dar es Saalam ambayo ni mahususi kwa malezi na masuala ya kijamii.
Kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo alikuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo alishika nafasi muhimu za kibiashara na kiuchumi:
Alihudumu
kama Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara na Uwekezaji katika Bunge hilo.
Pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira.
.........................
Katika nafasi hizo, alisimamia tofauti za
kiuchumi na maendeleo baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
jambo linaloonesha uzoefu wake katika kusimamia sera za kiuchumi.
BAADHI YA VIONGOZI WAELEZA UWEZO WAKE
Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa wa Jumuiya ya
Wazazi CCM na Diwani wa Kata ya Tabata, Sudi Kassim Sudi amesema Kizigha ni
kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kutokana na kushika nafasi mbalimbali ndani ya
chama.
“Kuna mambo ambayo tunajivunia kuhusu utumishi wake, ameshakuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hii Wilaya ya Kinondoni, Mjumbe wa Baraza Kuu kupitia Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, kwa nafasi hizi ana uzoefu mkubwa ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla, " alisema Sudi.
Akizungumzia kuhusu uteuzi wa Kizigha
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Ramadhan Madabida amesema ulizingatia muongozo wa mamlaka ya uteuzi.
“Ni lazima tuzingatie mamlaka ya uteuzi, mamlaka ya
uteuzi haifanyi kazi hivi hivi, uteuzi ni mchakato ‘process' na ofisi ya Rais
si mtu ni taasisi, kabla hajafanya uamuzi anashauriwa au kushauriana na vyombo
mbalimbali vinavyo mshauri.
''Kwa muktadha huo, uamuzi wowote anaoufanya lazima utakuwa umezingatia sifa, vigezo na uwezo wa mtu husika, kwa hali hiyo mimi sina mashaka kabisa kwamba katika kuteuliwa kwake hayo yalizingatiwa na uamuzi ukafikiwa kwamba anafaa kufanya kazi hiyo,” alisema Madabida.
Madabida aliongeza kuwa Kizigha alishawahi
kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Bunju, ameshawahi kuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dar
es Salaam.
Alisema alipokuwa kwenye nafasi hizo yeye
akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam hakuwa na wasiwasi wowote wa
kumtilia shaka uwezo wake.
“Alifanya kazi zake kwa uwezo mkubwa, kwa kujitolea nguvu zake, akili zake na rasilimali zake bila kusita na ni mtu ambaye Waingereza wanamuita mwenye "High Emotional Quotient" mtu ambaye anauwezo wa kujichanganya kwenye mazingira yoyote na wakamkubali na kumuona kama miongoni mwao wasiwe na wasiwasi naye na kushirikiana naye," alisema Madabiba.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya
kuwania Urais wa Tanzania, Hayati Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye
Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu Juni 27, 2015, akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate
ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
.........................
Aliongeza kuwa nafasi hiyo aliyopewa inaendana na uwezo wake na hulka zake na kuwa hana shaka naye ataweza kuifanya kama anavyotakiwa afanye na ataisaidia mamlaka iliyomteua katika kufikia malengo yale ambaayo anakusudiwa hayafikie.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, uteuzi huo unalenga kuimarisha ushauri wa
kisera katika masuala ya kijamii yanayogusa ustawi wa wananchi.
Mhe. Kizigha
anatasaidia katika kuratibu na kushauri kuhusu programu na mikakati ya kijamii,
ikiwemo maendeleo ya jamii na ustawi wa makundi mbalimbali.
Uteuzi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha utendaji kazi katika ngazi ya juu ya maamuzi ya Sera.
MAJUKUMU YA MSHAURI WA MASUALA YA KIJAMII
Kwa ujumla,
majukumu ya mshauri wa masuala ya kijamii yanahusisha mambo kadhaa yafuatayo:
Ushauri wa
Sera: Kutoa mwongozo kuhusu masuala ya ustawi, haki za binadamu na maendeleo
ya jamii.
Utatuzi wa
Migogoro: Kusaidia kurekebisha changamoto zinazoibuka ndani ya jamii au vikundi
mbalimbali.
Ufuatiliaji
na Tathmini: Kupima ufanisi wa programu za kijamii zinazotekelezwa na serikali
au mashirika.
Ushawishi
(Advocacy): Kutetea makundi yenye mahitaji maalum kama watoto, walemavu, na
wazee.
Majukumu ya
mshauri wa masuala ya kijamii (Social Affairs Consultant/Advisor)
yanatofautiana kulingana na mazingira ya kazi (ngazi ya taifa, mradi, au
shirika la kimataifa), lakini kwa ujumla yanajikita katika kuhakikisha ustawi
wa watu, ushirikishwaji wa jamii, na uzingatiaji wa haki za binadamu katika
mipango ya maendeleo.
Yafuatayo ni majukumu ya msingi ya mshauri wa masuala ya kijamii kulingana na vyanzo:
1. Ushirikishwaji wa Jamii na Uhamasishaji
Mshauri ana jukumu la kuwa kiungo (catalyst) au mhamasishaji wa jamii ili kusaidia wananchi kutambua fursa na changamoto zinazowakabili.
Majukumu hayo ni pamoja na:
Kushirikisha
jamii katika kuibua, kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia
mbinu shirikishi.
Kuelimisha
jamii kuondokana na fikra, imani, mila, na desturi zinazokinzana na maendeleo
au zinazoleta ukatili.
Kuandaa miongozo na jumbe rahisi zinazoelezea sera na mipango ya kitaifa ili jamii iweze kuzielewa na kuzitekeleza.
2. Kinga za Kijamii na Usimamizi wa Riski (Social Safeguards) Katika miradi mikubwa ya kitaifa au ya kimataifa (kama ya Benki ya Dunia au ADB), mshauri huhakikisha kuwa mradi hausababishi madhara kwa jamii.
Kazi hizi ni pamoja na:
Kufanya
tathmini ya athari za kijamii (Social Impact Assessment) kabla na wakati wa
utekelezaji wa miradi.
Kusimamia
masuala ya uhamishaji wa watu kwa lazima (Involuntary Resettlement) na
kuhakikisha fidia stahiki inatolewa.
Kuhakikisha uzingatiaji wa sheria za kazi na viwango vya kimataifa vya usalama wa jamii katika maeneo ya miradi.
3. Maendeleo ya Jinsia na Makundi Maalum
Mshauri ana wajibu wa kuhakikisha maendeleo ni jumuishi kwa makundi yote.
Hii inahusisha:
Kuratibu
uingizwaji wa masuala ya jinsia katika programu na mipango ya maendeleo ya
kisekta.
Kukusanya na
kutafsiri takwimu za mchanganuo wa kijinsia ili kubaini mapungufu yaliyopo.
Kuwaunganisha na kuwawezesha wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu kupata fursa za kiuchumi, mikopo, na stadi za maisha.
4. Ulinzi na Haki za Watoto
Katika ngazi
ya kitaifa na jamii, mshauri husaidia kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Mtoto na
Sheria ya Mtoto.
Majukumu ni pamoja na:
Kuelimisha
jamii kuhusu haki za msingi za mtoto (kuishi, kulindwa, na kushirikishwa) na
malezi bora.
Kuratibu
uundaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa
ili kutoa sauti kwa watoto.
Kusimamia utekelezaji wa mipango ya kitaifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
5. Uratibu
wa NGOs na Wadau wa Maendeleo
Mshauri mara
nyingi hufanya kazi kama mratibu kati ya serikali na mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs).
MAKALA HII IMEANDALIWA NA DOTTO MWAIBALE SIMU NAMBA 0754362990 / EMAIL : DOTOMWAIBALE@GMAIL.COM










0 Comments