Na Dotto Mwaibale, Dodoma
Mwasisi wa Kigoda cha
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Mtandaoni, Balozi wa Amani Tanzania na
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Kata ya Iganjo Jimbo la Uyole
Jijini Mbeya, Suma Oddo Lwena
amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya na kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (PhD), kutoka
Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa cha nchini Nigeria.
Shahada hiyo ya heshima alitunukiwa Aprili 11, 2026 kwa njia ya mtandao.
“ Kazi nzuri anayoifanya Rais wetu ndiyo sababu ya
kutunukiwa tuzo hiyo kwetu sisi kama nchi nimafanikio makubwa,” alisema Lwena.
Lwena aliongeza kuwa Shahada hiyo ya Heshima aliyotunukiwa ni kutokana na kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia, afya ya mama na mtoto, taswira nzuri katika masuala ya uongozi kwa wanawake Afrika na jinsi anavyosimamia masuala ya biashara hususani kwa vijana wa Afrika.
Mwasisi wa Kigoda cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Mtandaoni, Suma Addo Lwena.









0 Comments