KAMBI YA MAFUNZO SENETI VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA YAWA YA MAFANIKIO

KAMBI YA MAFUNZO SENETI VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA YAWA YA MAFANIKIO


Katibu wa Hasama wa Seneti ya Vyuo Vikuu na Vyuo Mkoa wa Dodoma, Ajoki Mwakatebe akizungumza wakati wa Kambi Maalumu ya Mafunzo inayoendelea mkoani humo ambayo itafikia tamati Aprili 9, 2026.

...............................

KAMBI ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma imekuwa na mafanikio kufuatia washiriki kujitokeza kwa wingi licha ya wanafunzi wengi kuwa kwenye likizo.

Katibu wa Hasama wa Seneti hiyo Mkoa wa Dodoma, Ajoki Mwakatebe akizungumzia kambi hiyo     alisema ni kwa ajili ya  mafunzo maalumu ya siku tatu ambayo imewahusisha washiriki zaidi ya 440 wa mkoa huo.

 “Kambi hii ya siku tatu ilianza Aprili 7, 2026 na itafikia tamati kesho Aprili 9, 2026 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na maudhurio mazuri ya washiriki zaidi ya 440 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na isingekuwa wanafunzi kuwa likizo idadi ingekuwa kubwa zaidi ,” alisema Mwakatebe.

Mwakatebe alisema katika mafunzo hayo mada zilizotolewa zilihusu wajibu na majukumu ya vijana kwa CCM, Ujenzi wa hoja na matumizi ya mitandao na siasa za mitandao.

Alitaja maada nyingine kuwa ni dhana ya ujamaa katikaa siasa na uchumi wa kisiasa,  dhana ya kazi za chama, mahusiano kati ya chama na Serikali, itikadi na imani ya CCM na dhana ya ulinzi wa chama.

Aidha, Mwakatebe alitaja mada zingine kuwa ni maandalizi ya uchaguzi wa chama na jumuiya na Itifaki ya chama na jumuiya.

Alisema siku ya kwanza ya mafunzo hayo walianza na mdahalo ambao ulihusu nafasi ya kijana katika kuleta matokeo chanya ndani ya CCM na maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

Washiriki wakiwa kwenye kambi hiyo.

Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Moshi Mjini, Elisha Lundi akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Joel Kituu, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
 

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0755362990

Post a Comment

0 Comments