Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kibondo Hamisi Salumu Tahiro ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Kigoma akihutubia kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM 2026 yaliyofanyika Kiwilaya Kata ya Kizazi. Tahiro alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo,
.....................................
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma katika
kuadhimisha wiki ya Wazazi 2026 imeshiriki shughuli mbalimbali za kijamii
ikiwemo kufanya usafi na matendo ya huruma kwa wenye uhitaji.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Aprili 9, 2026 yalishirikisha
viongozi mbalimbali wa Serikali, CCM pamoja na Wananchi yakiongozwa na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Kibondo Hamisi Salumu
Tahiro ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Kigoma.
Tahiro akihutubia kwenye maadhimisho hayo alihimiza malezi kwa watoto na kudumisha mshikamano ambapo alitumia nafasi hiyo kupongeza juhudi za maendeleo alizozifanya Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Dkt. Florence Samizi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya ikiwemo kujenga Kituo cha Afya Kata ya Kizazi fedha kutoka Serikali Kuu zilizotolewa na Rais Samia na mchango wa mfuko wa jimbo sanjari na ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kasana.
“Kwa maendeleo haya tuliyoyapata tunamshukuru sana Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu
Hassani na mbunge wetu Dkt. Florence Samizi,” alisema Tahiro.
Aidha, Tahiro alihimiza utunzaji wa mazingira akieleza jambo hilo ni la muhimu sana na ndiyo maana moja ya ratiba yao katika maadhimisho hayo ilikuwa ni kufanya usafi.
Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kibondo, Evarist Msafiri akizungumza
kwenye maadhimisho hayo aliwataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia malezi
ya watoto wao hasa katika suala la maadili nakueleza kuwa vijana wengi siku
hizi wamekengeuka hivyo wasipofuatiliwa kwa karibu wataendelea kuharibikiwa.
“Jumuiya yetu ya wazazi jukumu lake kubwa ni kusimamia suala
zima la malezi, maadili na elimu hivyo ni vizuri tukawa jirani na watoto wetu kwa ajili
ya malezi yao badala ya kuwaacha wakiharibika,” alisema Msafiri.
Aidha, Msafiri alisema Maadhimisho hayo ya wiki ya Wazazi
2026 yamefanyika vizuri huku yakiwa na maudhurio makubwa ambapo alitoa
shukurani zake kwa wote waliojitokeza kushiriki na kueleza kuwa wameonesha
umoja na mshikamo mkubwa.
Alisema maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Kizazi Tarafa ya
Mabamba yalikuwa ya mafanikio kwani washiriki walijitokeza kwa wingi na kufanya
usafi katika viunga vya Kituo cha Afya cha kata hiyo eneo la Nyalugusu.
Alisema mbali na kufanya usafi pia walitoa misaada kwa
makundi mbalimbali ya watu wenye Uhitaji wakiwemo wazee tukio lililofanyika kwenye mkutano
wa hadhara.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kizazi Benson Mahori
Bavuma alitumia nafasi hiyo kuelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo
iliyofanyika ikiwemo kituo kipya cha afya kilichojengwa na kuwa Serikali tayari
imepeleka watumishi ambao wanaendelea na kazi.
“Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia pamoja na
Mbunge Dkt. Florence Samizi kwa jitihada zao za kufanikisha maendeleo katika
maeneo yetu haya,” alisema Bavuma.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Kibondo, Evarist Msafiri akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Usafi ukifanyika kwenye viunga vya Kituo cha Afya Kata ya Kizazi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo, Hamisi Tahiro akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji.
Maadhimisho hayo yakiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Viongozi wakielekea eneo la sherehe
Maadhimisho yakiendelea
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Muonekano wa kituo cha Afya kilichojengwa na Serikali Kata ya Kizazi.
Usafi ukifanyika KKituo cha Afya Kata ya Kizazi.
Wakina mama wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.





















0 Comments