JUMUIYA YA WAZAZI CCM ILALA YAWAPONGEZA GONGOLAMBOTO, UKONGA

JUMUIYA YA WAZAZI CCM ILALA YAWAPONGEZA GONGOLAMBOTO, UKONGA

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi yaa Chama Cha Mapinduzi ((CCM), Wilaya ya Ilala, Mtiti Mbassa akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo wa Gongolamboto na Ukonga ,  AprilI 12, 06..

.......................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
  

 UONGOZI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, umewapongeza wananchi wa Kata ya Gongolamboto na Ukonga kwa kumchagua kwa kishindo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan. 

Dk. Samia alichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa urais, wabunge na madiwani uliofanyika Oktoba 29, mwaka jana. Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM), Wilaya ya Ilala, Mtiti Mbassa wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo,  AprilI 12, mwaka huu, kàtika kikao kilichofanyika Gongolamboto na Ukonga, 

 "Nawapongeza jumuiya ya wazazi na wananchi wote kwa kumchagua Rais Dk. Samia, mbunge na madiwani na kuwezesha CCM kuunda serikali," alisema Mtiti.

Mtiti alisema sifa ya CAM ni kuunda serikali na sasa kilichopo mbele yetu ni kuchapa kazi.         Kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo, inafanya ziara katika kata 36 za Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuwakumbusha viongozi wa matawi kuimarisha uhai wa jumuiya na chama. 

Katika kikao hicho cha kiutendaji kilihudhuriwa na viongozi wa serikali akiwamo watendaji wa kata wa Gongolamboto na Ukonga, maofisa elimu, ustawi wa jamii na afya.

Wengine ni walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, kamati za shule na bodi za shule.                 

Kwa upande wa chama waliohudhuria kikao hicho ni viongozi wa mashina ya CCM, jumuiya ya wazazi ngazi ya matawi, wanachama na viongozi wa kata. 

Mtiti alisema lengo la kuwaita viongozi hao ni kujadiliana na kusikiliza kero ya elimu kwa shule za msingi na sekondari kama inayoelekeza kwenye kanuni za jumuiya hiyo. 

Alisema jumuiya ya wazazi ndiyo yenye majukumu mengi ya kama kanuni inavyoelekeza.     Jumuiya ya wazazi inahusika kusimamia malezi na mazingira, elimu, afya, maadili ya Taifa na utamaduni. 

Pia aliwataka viongozi jumuiya ya wazazi ngazi ya matawi kuongeza idadi ya wanachama na kuhakikisha wanalipa ada. 

Mtiti alisema baada ya kufanikiwa kuunda serikali hiki ni kipindi cha kufanya kazi na hatakubali baadhi ya watu wanafanya vikao bila kufuata utaratibu kwa mujibu wa kanuni.  Alisema vikao vyote vya jumuiya ya wazazi vinatakiwa kufanyika kwa kufuata utaratibu na si vinginevyo. 

Baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao hicho,  akiwamo Afsa Elimu wa Kata ya Ukonga, Anita Mwangamila,  alisema wamefurahi kupata somo kuhusu kazi zinazofanywa na jumuiya hiyo na kuahidi kuanza utekelezaji ili kuendana na mpangokazi na ratiba za vikao.

Post a Comment

0 Comments