Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala, Mtiti Mbassa, akizungumza kwenye muendelezo wa ziara zake.
..........................
UONGOZI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, umewataka viongozi ngazi ya matawi kuhitisha mkutano wa wanachama wote wa jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa kanuni za Jumuiya ya Wazazi CCM, kila baada ya miezi minne wanatakiwa kufanya mikutano hiyo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala, Mtiti Mbassa, alitoa agizo hilo jana katika mwendelezo ya ziara yake katika kikao kilichofanyika Kata ya Buguruni, jijini Dar es Salaam.
Mtiti na wajumbe wake wa kamati ya utekelezaji wanaendelea na ziara ya kiutendaji kuhusu kuimarisha jumuiya na chama kwa mujibu wa kanuni.
Alisema viongozi wa jumuiya ya wazazi ngazi ya matawi tangu wachaguliwe mwaka 2022 hawajahitisha mkutano wa wanachama kwa mujibu wa kanuni ya jumuiya hiyo.
Katibu huyo wa Jumuiya ya Wazazi CCM, alisema kwa mujibu wa kanuni, viongozi walitakiwa kuhitisha mkutano wa wanachama, jambo ambalo halijafanyika.
"Nimetoa ratiba ya vikao na kila tawi linatakiwa kufanya mkutano wa wanachama wote mwezi huu,".
" Tangu mwaka 2022 hakuna mkutano wa wanachama uliofanyika kwa mujibu wa kanuni, sisi viongozi hatuwatendei haki wanachama," alisema Mtiti.
Katika kikao hicho, Mtiti alisisitiza usajili wa wanachama wapya kupitia mfumo wa TEHAMA na ulipaji wa ada wa wanachama.
Mtiti alisema anatoa maelekezo ya kufanya vikao na kujikuta mnawaalika wenyeviti wa serikali za mitaa, kamati za shule, mashina na viongozi wengine katika mikutano yenu.
Pia, Mtiti alisema Jumuiya ya Wazazi CCM ipo kiutendaji zaidi, hivyo inajukumu la kusimamia sekta ya elimu, afya, maadili ya taifa, malezi, utamaduni na mazingira.
Ziara hiyo iliyoanza Aprili, 7, mwaka huu, inahusisha Kata 36 za Wilaya ya Ilala, ikiwa ya kikazi zaidi









0 Comments