..................................
Na Mwandishi Wetu, Kagera
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan amesisitiza juhudi za pamoja za kuboresha miundombinu ya michezo ya Shule ya Msingi Kitunga iliyopo Kata ya Muhutwe wilayani Muleba mkoani Kagera ili kuongeza hamasa na hamu zaidi ya ushiriki wa jamii katika michezo.
Faris ameyasema hayo akizungumza hivi karibuni kama mgeni rasmi wakati wa mchezo wa fainali wa mashindano ya mpira wa miguu ya Ramadhan Coffee Cup iliyoshirikisha timu 16 kwenye wilaya ya Muleba, iliyofanyika katika uwanja wa shule hiyo, Kitunga Arena.
Amesema juhudi zinahitajika kuboresha uwanja wa mpira wa miguu wa shule hiyo kutoka kwenye milingoti ya mbao ya muda na kuweka milingoti ya kudumu ya chuma.
Ili kufanikisha maboresho hayo, Faris ameratibu ahadi za kifedha kutoka kwa Mbunge wa eneo hilo, huku yeye mwenyewe akichangia fedha kwa ajili ya nyavu za kisasa za michezo na vifaa vya uratibu wa mashindano.









0 Comments