DIWANI MKWESE ATOA MIPIRA BONANZA LA PASAKA MANYIGU FC

DIWANI MKWESE ATOA MIPIRA BONANZA LA PASAKA MANYIGU FC

Diwani wa Kata ya Mkwese , Shigela Ngwigulu (Aliyeshika mpira), akiwa na wachezaji wa Timu ya Manyigu FC Mbweko ambayoitafanya Bonanza la Pasaka katika Kata hiyo leo Aprili 5, 2026.

............................................

Na Dotto Mwaibale

DIWANI wa Kata ya Mkwese , Shigela Ngwigulu ametoa mpira kwa Timu ya Manyigu FC Mbwekoo inayotarajia kuwa na Bonanza la siku ya Pasaka katika kata hiyo leo Aprili 5, 2026..

Akizungumza wakati akiwakabidhi mpira Ngwigulu amewaasa vijna hao kutunza afya zao na kuacha kuwa walevi wa michezo ya bahati na sibu kama mabonanza na kamali na kijikita katika michezo ili kuwa na taifa imara, 

Shigela ameendela kuligusa kundi la vijna huku akisisitiza kulinda nchi nchi yetu  kwani hatuna Tanzania nyingine hivyo ni wajibu wa Kila kijana.

Aidha,  amewaasa vijna kulinda amani ya Kata ya Mkwese na Wilaya ya Manyoni na kusisistiza kuwa makamanda wa kumlinda Dkt Samia suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Gimu Ntandu alimshukuru diwani huyo kwa kudhamini bonanza hilo kwa ajili ya vijana wa kata hiyo.

"Tunashukuru sana Mhesshimiwa diwani wetu kwa kudhamini bonanza letu na kutupatia mpira na vifaa vingine vya michezo ni jambo jema sana kwetu sisi Mungu akubariki kwani michezo ni afya na ajira,"alisema Ntandu..

 

Post a Comment

0 Comments