UVCCM WILAYA YA DODOMA MJINI ZIARANI KATA YA MAKULU

UVCCM WILAYA YA DODOMA MJINI ZIARANI KATA YA MAKULU

Katibu UVCCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Mengi Mwakisole.

....................................

Na Dotto Mwaibale, Dodoma 

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Dodoma Mjini wakiongozwa na Katibu wao Mengi Mwakisole wanatarajia kufanya ziara ya kiutendaji Kata ya Dodoma Makulu jijini humo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Idara ya Habari ya Umoja huo ziara hiyo itafanyika kesho Jumamosi Februari 21, 2026 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi, hivyo vijana wote wa umoja huo watatakiwa kuelekea Makulu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwakisole alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua uhai wa jumuiya hiyo ngazi ya matawi, kata, kusikiliza changamoto za vijana na kukumbushana juu ya  kutekeleza wajibu wa Viongozi.

Mwakisole ametumia nafasi hiyo kuwaomba vijana wa jumuiya hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki ziara hiyo ambayo ni ya muhimu,

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990 

Post a Comment

0 Comments