MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA, MAGANYA ATOA MAAGIZO MAZITO SEKONDARI YA HOMBOLO DODOMA

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA, MAGANYA ATOA MAAGIZO MAZITO SEKONDARI YA HOMBOLO DODOMA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Taifa, Fadhili Maganya (mwenye skafu) akipata maelezo  alipotembelea Shule ya Sekondari Hombolo iliyopo Kata ya Hombolo Bwawani Januari 14, 2026 mkoani Dodoma.

..................................

Na John Banda, Dodoma

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Taifa, Fadhili Maganya ametoa maagizo kwa viongozi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari kuonana nae kwa njia yoyote ile baada ya kushindwa kufika katika eneo la tukio ingawa walipata taarifa za ujio wake katika shule hiyo.

Maganya ametoa tamko hilo hiyo anuari 14,2026, alipotembelea Shule ya Sekondari Hombolo iliyopo Kata ya Hombolo Bwawani na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya shule kwa niaba ya wanafunzi wote nchini.

Akitoa Maagizo hayo amesema kuwa hawezi kufika katika shule hiyo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya shule na hawapo jambo hilo haliwezi kuvumika.

” Sasa nitawalekeza waje wakiwa wanakimbia na ninataka ndani ya wiki mbili hapa si ni jiji hata kama ingekua ni kijijini ndani ya wiki mbili mwenyekiti wa bodi,mkuu wa shule muwe mmeshakwisha kupata hati ya umiliki wa eneo hilo sawa manake shule zingine hua zina maeneo mengi kwa sababu kama hapatakuwa na mipaka ni rahisi wananchi kumega kidogo kidogo halafu baadae mnaishia kugombanagombana” Amesema hayo Mwenyekiti wa CCM Taifa Maganya.


Vijana wa Itifaki wa CCM wakimvika skafu Mhe. Maganya baada ya kuwasili kutembelea shule hiyo.

Ziara ya kutembelea shule hiyo ikiendelea.

Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa ukumbini kwa ajili ya kupata ujumbe wa ugeni huo.
Mhe. Maganya akiwa meza kuu na viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
 

Post a Comment

0 Comments