............................................
Na Dotto Mwaibale
TAWI la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Seneti ya Mkoa wa Dodoma Tawi la CIVE Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), chini ya Mwenyekiti wake Meshack Kondowe kinatarajia kufanya darasa la Itikadi kwa wanachama wake wote.
Akizungumza na waandishi wa habari Kondowe alisema lengo kuu la darasa hilo ni kuwaandaa vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kuwajengea uelewa juu ya Sera na misingi ya Chama Cha Mapinduzi, Umuhimu wa mshikamano wa vijana katika siasa, maendeleo ya Taifa na nafasi ya vijana katika kushiriki kikamilifu uchaguzi na kuilinda amani ya nchi yetu.
Kondowe alisema darasa hilo litafanyika Agosti 23,2025 kuanzia saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa LRB 004C
" Nitumie nafasi hii kuwahimiza washiriki wote kufika mapema kuhudhuria darasa hilo kwani ni fursa kwao tukizingatia kuwa vijana ndio chachu ya ushindi na maendeleo ya Taifa letu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Seneti ya Mkoa wa Dodoma Tawi la CIVE Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Meshack Kondowe.










0 Comments