Msimamizi wa Uchaguzi wa INEC katika majimbo ya Segerea, Kivule, Ukonga na Ilala, Faraja Nakua. akimkabidhi fomu Mgombea Ubunge Jimbo la Segerea Bonna Kamoli jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2025.
......................................
MAELFU ya wanachama, wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi katika Jimbo la Segerea, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, wamejitokeza kumsindikiza Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bonna Kamoli, kuchukua fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wilayani humo.
Msafara mrefu wa magari, pikipiki na bajaji wa mgombea huyo uliopambwa kwa shamrashamra, ngoma, matarumbeta na nyimbo za kuisifu CCM ulianzia katika eneo la Tabata Shule, majira ya saa 6:00 mchana, kupitia Tabata Segerea, kisha kuingia Barabara ya Segerea-Majumba Sita na kuingia Barabara ya Nyerere kisha Mtaa wa Lumumba zilipo ofisi ndogo za INEC.
Bonnah, alipanda gari linalofunguka kwa juu na kujitokeza katika paa la gari hilo huku akipunga mkono na kupeperusha bendera ya CCM katika mitaa msafara huo ulipopita.
Mgombea huyo alikabidhiwa fomu na Msimamizi wa Uchaguzi wa INEC katika majimbo ya Segerea, Kivule, Ukonga na Ilala, Faraja Nakua.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Bonnah aliwaomba wananchi wa Segerea kumpa kura nyingi na za kishindo mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan na yeye mwenyewe.
Bonna Kamoli akionesha begi lenye fomu baada ya kukabidhiwa.
Maandamano na shamrashamra za uchukuaji wa fomu zikiendelea.
Taswira ya maandamano ya tukio zima la uchukuaji








0 Comments