KIHONGOSI AANZA KAZI RASMI

KIHONGOSI AANZA KAZI RASMI

Kuongoza kikao cha maandalizi ya uzinduzi kampeni Sinza Dar es Salam leo

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Kenani Kihongosi.

.................................

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Kenani Kihongosi ameanza kazi rasmi na leo leo anatarajia kuongoza kikao kazi cha viongozi wa ngazi ya kata na jumuiya ya chama hicho.

Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupanga mikakati ya maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za kitaifa zitakazo zinduliwa Agosti 28, 2025 na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan viwanja vya Tanganyika Peackers Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu Katibu  wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga alisema maandalizi yote ya kikao kazi hicho yamekamilika na kitaanza Saa 4:00 asubuhi.

“Hiki ni kikao cha kwanza kukifanya Katibu wetu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi tangu Kikao cha Halmashuri Kuu ya CCM (Taifa) kilichoketi Agosti 23, 2025 na kumteua kushika nafasi hiyo,” alisema Bananga.

Alisema kikao kazi hicho kinafanyika Ukumbi wa Mawela Sinza. Katibu  wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga 


Post a Comment

0 Comments