Na Dotto Mwaibale
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi leo wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Asha- Rose Migiro atapowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Dkt. Migiro anatarajiwa kuwasili katika ofisi hizo kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Kikao cha Halmashuri Kuu ya
CCM (Taifa) chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.Samia Suluhu Hassan kilichoketi Agosti 23, 2025 kilimteua
Dkt. Migiro (Balozi) kushika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho.
Wananchi na wana CCM wanakaribishwa kushiriki katika tukio hilo la kihistoria ambapo Dkt. Migiro anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.









0 Comments