WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamempongeza Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa huo Bi, Subira Mgalu kwa namna anavyopigania maendeleo na kumuelezea kuwa ni kiongozi ambaye anawiwa kuwatumikia na ni Lulu kwao.
Pongezi hizo wamezitoa katika hafla ya kumtunuku cheti maalumu cha pongezi kutambua mchango wake wa kuwatumikia wananchi na UWT iliyofanyika jana wilayani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
"Jinsi ambavyo Mbunge Mgalu amekuwa akijitoa kwenye masuala mbalimbali ya kijamii pasipo kujali dini wala kabila inaonesha ni kiongozi mwenye moyo wa kuwatumikia wananchi na hasa UWT," alisema mmoja wa wanachama wa CCM.
Naye, Mwanahawa Hamja ambaye ni Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Bagamoyo amempongeza Mhe Mgalu kwa kusaidia Jumuiya kwa kiwango cha hali ya juu katika masula mbalimbali ila kubwa ni la kutoa gari kwa lengo la kusaidia viongozi ili waweze kuwafikia wanachama wa ngazi za chini.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Ramadhani Lukanga alisema kuwa Mhe Mgalu amekuwa nguzo imara sana katika kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo ndio maana ametoa gari kwa ajili ya kwenda kuwafikia wanachama kwa wepesi.
Aidha, amemtaka kuendelea kuwa na moyo huo wa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kupata ushindi mnono kwa kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Madiwani








0 Comments