MLEZI WA UVCCM TAWI LA TIA DAR ES SALAAM AHIMIZA KUJITOKEZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA

MLEZI WA UVCCM TAWI LA TIA DAR ES SALAAM AHIMIZA KUJITOKEZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA

Leo Mei 16, 2025 Mlezi wa Tawi la UVCCM TIA Dkt Isaya Hassanal ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Fedha, Mipango na Utawala wa Taasisi ya Uhasibu wa Tanzania (TIA) ametoa salamu kwa Vijana Kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura lakini pia amewahamasisha Vijana kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

 " Natoa wito kwenu muende  kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili muweze  kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 2025 kwa kugombea ama kuwachagua viongozi bora ambao watatuwakilisha vyema katika jamii na taifa letu" alisema

Dkt Hassanal ameyasema hayo katika baraza la wanafunzi lenye lengo kusikiliza changamoto zinazowakumba wanafunzi wa chuo hicho pamoja na kuzipatia ufumbuzi.

Post a Comment

0 Comments