...........................................
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko tarehe 27 Aprili, 2025 amefanya ziara, pamoja na mambo mengine amekabidhi picha za Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ofisi za UWT Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, akiwa ameambatana na Kamati za Utekelezaji za UWT Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro, Esther Edwin Malleko ametembelea wodi za Wanawake hospitali za Wilaya ambapo amekabidhi Sabuni kwaajili ya Mama Wajawazito na Watoto.
Vilevile, Esther Edwin Malleko katika kuwainua kiuchumi wanawake wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro, amekabidhi Mashine za kutotoresha vifaranga vya Kuku kwa Kamati za Utekelezaji za UWT Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Mwisho, Esther Edwin Malleko amewataka wananchi, viongozi wa UWT na wana UWT wote wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kishindo katika Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.









0 Comments