Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM Taifa Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC), ameshiriki katika siku ya pili ya mwendelezo wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, leo tarehe 30 Mei 2025.
Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025–2030, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu 2025, na kufunga rasmi Mkutano huo Maalum.








0 Comments