Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya UVCCM Taifa Ndugu Rehema Sombi Omary MNEC amesema ni kazi ya Vijana Kulinda na Kutangaza juhudi zinazofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi.
Ameyasema hayo alipokua akizungumza na Vijana pamoja na Wanachama waliojitokeza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mtekelezo Jijini Dodoma ikiwa ni Uzinduzi wa KIJANI FIRST VOTERS , Leo 24 Mei,2025,
Ndugu Rehema amesema ni wajibu wa Vijana kuilinda Amani iliyopo Nchini na Wasiwe tayari kutumika na Makundi wenye nia ovu kwa Taifa letu.
Pia amewataka Vijana kua Mstari wa mbele katika kuchukua fomu za kugombea katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 .
Vilevile amempongeza Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC) Pamoja na Kamati Tekelezaji Taifa kwa kuendelea Kua Mstari wa Mbele katika Kuhakikisha Rangi ya Kijani Inaenea Na Kustawi Nchi nzima kwa Kuyaelezea Mema Yote yanayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Aidha amesema UVCCM kwa umoja wao Wamekubaliana Kumpatia Ushindi wa Kishindo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ifikiapo Oktoba 2025.








0 Comments