Afisa Tarafa (Gavana) wa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku Bwanku akitoa mada inayohusu utawala bora kwenye Sherehe ya Uzinduzi wa Wiki ya Wazazi ambayo kimkoa wa Kagera ilifanyika Kemondo Tarafa ya Katerero Aprili 14, 2025.
.............................................
Na Mwandishi Wetu, Kagera
Afisa Tarafa (Gavana) wa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku Bwanku aliwaongoza watoa mada kwenye Sherehe ya Uzinduzi wa Wiki ya Wazazi Mkoa wa Kagera wakati wa Kongamano la Maadili lililofanyika Ukumbi wa Bukoba Resort uliopo Kemondo Tarafa ya Katerero.
Gavana Bwanku akiwasilisha Mada kuhusu Utawala Bora alieleza kwa kina Dhana nzima ya Utawala Bora na jinsi Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza kwa vitendo dhana hiyo kwa uwajibikaji kwa umma kwa kutekeleza wa miradi mbalimbali ya maendeleo kote nchini ili kuleta ustawi wa jamii na kukua kiuchumi kama lengo kuu la dhima ya Utawala Bora.
Maadhimisho hayo yanaendelea maeneo mbalimbali nchini ambapo katika Mkoa wa Kagera uzinduzi wake ulifanyika Aprili 12,/2025 Tarafa ya Katerero ukiambatana ufanyaji wa shughuli za kupanda miti 200 Shule ya Msingi Kanazi B, kutembelea Kituo cha Watoto yatima Bethania Children's Home na kutoa zawadi pamoja na kufanya Kongamamo hilo.
Watoa mada katika kongamano hilo walitoka katika taasisi zilizo chini a Serikali kama Ofisi ya Afisa Tarafa Katerero, Ofisi ya Afisa Elimu wa Mkoa, Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera (Dawati la Jinsia) Mganga Mkuu wa Mkoa, Udhibiti Ubora Mkoa na Takukuru Mkoa huku mgeni rasmi akiwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Kagera Comrade Hamimu Mahmudu.
Aidha, Gavana Bwanku kwenye sherehe hiyo alitoa miti ya matunda na kuigawa kwa Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kutoka kata zote 29 za Bukoba Vijijini ili wakaipande huku akihamasisha kwenda kutunza mazingira kama ilivyo jukumu lake kubwa la Jumuiya hiyo wakati huu Serikali ikihamasisha sana upandaji wa miti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ukame, jangwa n.k
Upandaji wa miti ukifanika

Watoto yatima wakisalimiwa na kupatiwa zawadi mbalimbali.
Afisa wa Polisi kutoka dawati la jinsia akitoa mada inayohusu kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.
Taswira ya uzinduzi wa maadhimisho hayo sanjari na kongamano hilo.















0 Comments