Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) washiriki kuhamasisha kujiandikisha daftari la kudumu la wapiga kura Muheza mkoani Tanga.
.................................................
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Idadi kubwa ya wananchi wa Muheza wamejitokeza kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni matokeo ya hamasa kubwa inayoendelea kufanywa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) kwa kushirikiana na viongozi wa Chama na Serikali katika Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Zainabu Abdallah Issa.
Chatanda, ameyasema hayo leo tarehe 13 Februari, 2025
Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga alipokuwa akihamasisha Uandikishaji wa Daftari la
Wapiga Kura lililoanza leo tare 13 hadi 19 Februari, 2025 kwa Mkoa wa Tanga na
Pwani kwa kupita kwa Mabalozi wa Mashina, kujionea hali na mwamuko mkubwa
kwenye vituo vya kujiandikisha pamoja na kufanya Kongamano kubwa lililoandaliwa
na UWT Wilaya ya Muheza
Uhamasishaji ukiendelea.
Taswira ya uhamasishaji huo.













0 Comments