Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Hapi (MNEC), akihutubia mamia ya wananchi na wana CCM wa Bukoba katika Uwanja wa Kashai.
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Kagera
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Hapi (MNEC) amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine kufanya kampeni za
kistaarabu na kiungwana ili kuendelea kulinda amani na mshikamano uliopo nchini
huku akihamasisha wagombea kujikita katika kueleza sera zao badala ya kutumia
majukwaa kueneza siasa za chuki.
Hapi, amehutubia mamia ya wananchi na wanaccm wa Bukoba katika Uwanja wa
Kashai, akihamasisha umuhimu wa kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27
mwaka huu.
Katika hotuba yake, Hapi alisisitiza kuwa viongozi wa CCM wamekuwa na
rekodi bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
miundombinu ya elimu, afya, na maji chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu
Hassan.
Msafara wa pikipiki katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Hapi (MNEC)
Taswira ya mkutano huo.











0 Comments