Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda (MCC) akimnadi mmoja wa wagombea uongozi kwenye kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Riverside, Kata ya Mwembesongo mkoani Morogoro Novemba 24, 2024.
................................
Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda
(MCC) amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina imani kubwa sana na wanawake
na kinaamini wanamchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Taifa.
Chatanda amayasema hayo alipokuwa akizungumza na
wananchi wa Mtaa wa Riverside, Kata ya Mwembesongo waliojitokeza kwenye kampeni za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa hii leo.
Hata hivyo, Chatanda ameendelea na kampeni zake
za Mtaa kwa Mtaa, Nyumba kwa Nyumba, Mguu Kwa Mguu huku akielezea mafanikio
makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu
Hassan.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda (MCC), akihutubia kwenye mkutano huo.
Vijana wa UVCCM wakishangilia kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.












0 Comments