Pamoja na kupokea ugeni huo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020/ 2025.
Aidha, Kikwete amewakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la ukaazi na kupiga kura na kuwahimiza kuendelea kuamini kuwa serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasan bado inaendelea kutekeleza majukumu yake vizuri.
"Wana Bagamoyo tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mh.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa aliyotufanyia ya kutuletea maendeleo," alisema Kikwete.
Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe.Ridhiwani Kikwete, akiteta jambo na MNEC Ally Hapi wakati wa ziara hiyo.








0 Comments