...............................
Na Mwamvua Mwinyi, KIBAHA
UMOJA wa wanawake Kibaha Mjini, unatarajia kufanya Kongamano kubwa la
kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Taifa ,Dkt.Samia kwa
utekelezaji wa ilani kwa kuwawezesha na kutetea haki za wanawake.
Aidha umelaani vitendo vya unyanyasaji, ubakaji na ulawiti ,vinavyoendelea
kufanywa na baadhi ya wanaume wasiokuwa na aibu.
Akizungumza na Baraza la UWT wilaya na wajumbe wa kamati ndogondogo,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elina Mgonja alifafanua kuwa, Kongamano hilo
litafanyika kwenye uwanja wa Mailmoja Stand ya Zamani.
Alisema ,kwasasa maandalizi yanaendelea kufanyika ili kufanikisha jambo
hilo.
“Tunatarajia kufanya Kongamano kubwa, kwakuwa Rais wetu na Mwenyekiti wa
CCM Taifa amekuwa akifanya kazi kubwa kuinua uchumi na maendeleo ya nchi ,
Hatuna budi kumuunga mkono kwa jitihada zake”
“Amekuwa na kasi ya ajabu kupeleka fedha kwenye kukamilisha miradi mikubwa
ya kimkakati kuhakikisha inakamilika kwa wakati, kukarabati na kujenga
miundombinu ya barabara, kufikisha umeme na maji kwenye maeneo mbalimbali, kupeleka
fedha katika Halmashauri zetu na kuwezesha wanawake kupata fursa za kujikomboa
kiuchumi “
Aidha Mgonja aliiasa Jumuiya hiyo ngazi ya matawi,shina,kata na wilaya
iende na kasi, ya viongozi wa ngazi ya Juu UWT na Rais Samia ili kuacha alama.
“Tutokeni Tutembee tusikae, tutembee tushawishi wanawake waingie katika UWT
na Chama ili kujiimarisha kuelekea katika chaguzi za serikali ya mtaa na
uchaguzi mkuu “alieleza Mgonja.
Vilevile alizitaka, kamati ndogo kufanya kazi na UWT kwani wamechaguliwa
ili waweze kusaidia katika ushawishi,ubunifu.
Pamoja na hayo, Mgonja aliomba wajumbe watunze maadili ya vikao ,
haiwezekani vikao vilivyo kikatiba vikadharauliwa .
Aliwaasa, Makatibu wa UWT kata wafanye kazi kwa kujiamini,watunze heshima
waliyopewa kwa kukitumikia Chama na Jumuiya.
Mgonja alisisitiza, Umoja,Upendo ambayo ndio nguzo, badala ya
kuchafuana,kufanyiana fitna ,chuki.
Katibu wa UWT mjini Kibaha ,Cecilia Ndalu aliwataka wanawake ,waendelee
kushikamana,kusaidiana na kushirikiana kwa kuchota mazuri yanayofanywa na
wenzenu na kujifunza ili kujiimarisha katika Jumuiya.









0 Comments