UWT WILAYA YA SINGIDA YATEMBELEA KATA TATU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

UWT WILAYA YA SINGIDA YATEMBELEA KATA TATU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT) wa Wilaya ya Singida, Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kata tatu za wilaya hiyo kwa ajili ya kukagua utelelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

..........................

Na Dotto Mwaibale

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida Vijijini imefanya ziara ya kiutendaji kwa kutembelea kata tatu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)_

Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo Zaiinabu Abdallah alizitaja kata zilizotembelewa kuwa ni ya  Mgori, Ngimu na Itaja na kuwa katika ziara hiyo aliambatana na kamati ya utekelezaji ya wilaya ambapo walifanikiwa kukagua utekelezaji wa ilani hiyo ya 2020/2025 kwa kukagua miradi ya maendeleo Kata ya Mgori ikiwemo miundo mbinu ya maji, Shule ya Mwanamwema Shein NA  madarasa,

Aidha Katibu  huyo alisema katika ziara hiyo walifanikiwa kukabidhi  gari la wagonjwa litakalo tumika katika Kituo Cha Afya Mgori huku hafla ya makabidhiano ya gari hilo ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Mbunge Amina Senge.

“Mambo yote haya yaliyofanyika katika kata hizi ni matunda yanayo tokana  na kazi nzuri anayoifanya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wote wa wilaya hiyo Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla,” alisema katibu huyo.

Diwani wa Kata ya Mgori Dhuma Said  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara alwa UWT wilaya hiyo kwa kutembea kata hiyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho ambapo naye alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia diwani huyo alimshukuru Mbunge wa jimbo hilo Ramadhani Ighondo kwa jitihada anazozifanya za kuwasemea wananchi wa jimbo hilo bungeni ambapo matunda ya hayo anayowasemea ndio hiyo miradi lukuki inayoendelea kutekelezwa na serikali katika jimbo hilo.

Diwani huyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanashiriki ipasavyo kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu na kuwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watashinda kwa kishindo.

Diwani wa Kata ya Mgori Dhuma Said akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
Katibu wa Mbunge Amina Senge akizungumza kwenye mkutano huo.
Muonekano wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mgori yaliyokaguliwa wakati wa ziara hiyo 
 

Post a Comment

0 Comments