Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah (mwenye baghalashia), akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa ukaguzi wa viti vipi katika Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
......................................
Na Hamida Kamchalla, Tanga
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimedhamiria kuinua uchumi mkoani humo pamoja na wananchi wake kupitia mapato yanayotokana na michezo, hususani mpira wa miguu.
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Ustaadhi Rajabu Abdallah amesema hayo leo alipokagua uwanja wa michezo Mkwakwani jijini Tanga baada ya kufanyiwa maboresho pamoja na kufungwa viti vipya.
Amesema maboresho hayo pia yatainua uchumi wa wanamichezo hasa waliopo katika klabu za mpira wa miguu za Mkoa ambazo ni Coastal Union na African Sports ikiwa ni pamoja na vilabu hivyo kutokwenda kucheza nje ya Mkoa kama wenyeji.
"Yote tunayofanya kwenye kuboresha uwanja huu, mechi za Coastal Union na African Sports hazihamishwi kituo kwenda nje, timu zote za mpira kuna mechi za nje na ndani, sasa kwenye Mkoa wetu vilabu vyetu hivi viwili vikubwa, haiwezekani mechi za nje zikachezwe nje na mechi na nyumbani pia zikachezwe nje" amesema.
Lakini pia uwanja huo utaleta mafanikio baada ya maboresho na kukidhi vigezo kwani hata viwanja vya Mikoa mingine vikipata changamoto ya kufungiwa vilabu vyao vitakwenda kuchezea uwanja huo, hivyo kuingiza mapato.
Ustaadhi Rajabu pia amewaasa wananchi mkoani humo kuwa na mioyo ya kizalendo hasa baada ya maboresho hayo kujenga tabia ya kwenda uwanjani kuangalia mechi ili kuchangia vilabu vyetu vitakapokuwa vinacheza.
"Maboresho haya hayataleta maana kama tunafunga viti vya kisasa na uwanja kupendeza, na wakati huo Coastal Union inacheza halafu watu wanabaki kuangalia mpira nyumbani kwenye tv nadala ya kuja uwanjani, tunafunga viti ili tuje uwanjani kuipa nguvu timu yetu" amesema.
Jumla ya viti 6500 vimefungwa uwanjani hapo ambapo Mwenyekiti amesema bado kuna eneo liko wazi ambalo tayari limeombewa viti 2500.
Uwekaji wa viti hivyo ukikaguliwaMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah
Ukaguzi wa Uwanja huo ukifanyika
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah, aakizungumza.

Furaha ikitamalaki wakati wa uwekaji wa viti hivyo katika uwanja huo.













0 Comments