Mkufunzi wa Masuala ya Uchumi na Siasa Cde. Mwalimu Nebukadreza Malekela wakati akitoa mada katika Mdahalo na Wanachuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba - Mufindi mkoani Iringa Februari 20, 2026.
.........................
Na Dotto Mwaibale
VIJANA nchini wametakiwa kuilinda amani ya nchi kwa mifano ya kuigwa kwa kuwa hakuna mtu wa kutusaidia kuilinda.
Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa Masuala ya Uchumi na Siasa Cde. Mwalimu Nebukadreza Malekela wakati akitoa mada kwenye Mdahalo wa Wanachuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba - Mufindi mkoani Iringa Februari 20, 2026.
“Vijana tunapaswa kuendelea kuilinda amani ya nchi yetu kwakuwa hakuna mtu atakayetusaidia kuilinda nchi yetu zaidi ya sisi wenyewe,” alisema Malekela.
Malekela aliwasisitizia vijana hao umuhimu wa kulinda Sovereignty ya nchi kwa kuwa ina muhimu sana na kutaja mambo kadhaa ambayo ni ya muhimu kuwa ni Ulinzi wa rasilimali za Taifa, Husaidia nchi kuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na nchi nyingine.
Alitaja mambo mengine kuwa huchochea Maendeleo endelevu hasa katika Afya, elimu ,viwanda na mazingira na kueleza kuwa nchi yenye sovereignty inapewa hadhi kubwa kimataifa mfano Tanzania.
Aidha, Malekela alitaja jambo lingine kuwa ni Uhuru wa kujiamulia mambo yake kama nchi (self determination).
Katika Mdahalo huo uliohudhuriwa na washiriki zaidi ya 700 mada kubwa ilikuwa ni "NAMNA GANI VIJANA WATAILINDA ROHO YA NCHI (SOVEREIGNTY )"
Mwalimu Malekela akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwenye mdahalo huo.









0 Comments