Mbunge wa Jimbo la Hanang Mhe Asia Halamga akiishiriki hafla fupi ya Mama lishe ya kuvunja mzunguko wa Mwaka 2025 iliyofanyika Desemba 30, 2025.

......................................

Na Dotto Mwaibale

KIONGOZI bora ni yule anayewajali wananchi wake na kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo, furaha na huzuni pasipo kuwabagua jambo ambalo linawafanya wawe pamoja kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa.

Mbunge wa Jimbo la Hanang Mhe Asia Halamga ni mmoja wa viongozi bora ambaye anaonesha njia kwa kuwajali wananchi wake katika masuala ya maendeleo, furaha na huzuni amekuwa nao bega kwa bega liwake jua inyeshe mvua yeye na wananchi wake.

Licha ya kuwa na umri mdogo kwa muda mfupi tangu awe kiongozi akiwa mbunge kupitia kundi la vijana na sasa mbunge wa jimbo tumeona mambo mengi aliyoyafanya na Mungu anavyoendelea kumpa kibali cha kuwatumikia wananchi kwa nidhamu na unyenyekevu mkubwa na siyo kwa kuigiza.

Tumemuona ambavyo amekuwa akishirikiana nao katika matukio ya huzuni kama misiba, shughuli za maendeleo na furaha ambapo Desemba 30, 2025 alishiriki hafla fupi ya Mama lishe ya kuvunja mzunguko wa Mwaka 2025 ambapo alichangia jumla ya Sh. Milioni 2 kwa ajili ya kuwaunga mkono ili waweze kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Jambo hilo siyo dogo kwani wahenga wanasema ukiwainua wanawake kiuchumi unakuwa umeliinua Taifa kutokana na umuhimu wao katika jamii.

Halamga jicho lake la maendeleo linaona mbali kwani anaunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ambaye anamatamanio ya kuona kila mtanzania anainuka kiuchumi kwa msaada wa viongozi mbalimbali kama Halamga ambao wanaonesha kuwiwa kuwatumikia wananchi kwa dhati na vitendo na siyo blabla.

Wanawake hao walitumia nafasi hiyo kumshukuru mbunge wao kwa msaada huo na kumtakia afya njema na heri yam waka mpya wa 2026

Wakati huo huo jana Desemba 31, 2025 Mbunge Halamga, alisherehekea ukaribisho wa mwaka mpya wa 2026 pamoja na watoto kutoka maeneo mbalimbali ya Kata ya Bassotu ambapo alikula nao chakula pamoja na kuwapatia vifaa vya shule madaftari na kalamu kwa ajili ya masomo yatakayo anza shule zitakapofunguliwa mwezi huu wa Januari.

 Diwani wa Kata ya Bassotu, Rose Kamili, alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake alioutoa kwa watoto hao.

Wanawake wakionesha mshikamano kwenye hafla hiyo.
Wanawake hao wakimzawadia zawadi mbunge wao Asia Halamga.
Mbunge wa Hanang' Mhe. Asia Halamga, akiwagawia juisi watoto wa Kata ya Basoutu katika hafla aliyoiandaa ya kukaribisha mwaka mpya wa 2026.
Mbunge wa Hanang' Mhe. Asia Halamga, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kata hiyo.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.