Na Dotto
Mwaibale
UONGOZI ni mamlaka au karama ya
kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.
Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi husika anaweza kuleta ushawishi kwa
watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa
matatizo ya wananchi au watu walio chini yake anao waongoza.
Yustina
Arcadus Rahhi Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Manyara ni kiongozi bora
ambaye anafanya kazi yake kwa kushirikiana na wananchi wote pasipo kuwabagua iwe
katika furaha, huzuni na shughuli za maendeleo na hawatengi bali anakuwa nao sambamba
akijua kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.
Kutokana na
uongozi wake bora uliotukuka Januari 1, 2025 aliwiwa kutembelea Hospital ya Wilaya
ya Mbulu kwenda kuwajulia hali wagonjwa na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni
kuwatakia kheri ya mwaka mpya wa 2026.
Jambo hilo siyo dogo linaonesha jinsi ya kiongozi bora anavyoshirikiana na wananchi wake ambao anawaongoza.
Mbunge Rahhi
kwa kuwa ni kiongozi anaye shirikiana na wananchi na viongozi wenzake mkoani
humo katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael
Semundu na Mbunge wa Mbulu Vijijini Dkt. Emmanuel Nuwas ambapo pia walitembelea Kituo cha Afya Dongobesh na kuwapa faraja kubwa
wagonjwa kwa kuzungumza nao na kuwapatia zawadi.
Kwa nyakati
tofauti viongozi hao wakizungumza na wagonjwa hao waliwasisitizia kuendelea
kuiamini Serikali yao ambayo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya
kuwaletea maendeleo.
Aidha,
viongozi hao walimpongeza na kumshukuru Mhe. Rais kwa namna ambavyo
anawathamini wananchi na watumishi wa Wilaya ya Mbulu nan chi nzima kwa ujumla
ambapo walitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumuombea.
Baadhi ya wagonjwa na jamaa zao walimshukuru mbunge huyo, mkuu wa wilaya hiyo na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Dkt. Emmanuel Nuwas kwa ukarimu waliowaonesha wa kwenda kuwajulia hali pamoja na kuwapa zawadi kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 na kumuelezea kuwa mbunge huyo kuwa anaacha alama ya kuwatumikia.
Mbunge Rahhi ni mama mpole, mwenye huruma na mpenda maendeleo na mchapa kazi ambapo tangu ashike nafasi hiyo amekuwa na mchango mkubwa katika Mkoa wa Manyara na michango yake bungeni imekuwa ikionekana na kuleta tija.







0 Comments