Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbinga, Joseph Mdaka, akiongoza kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya chama hicho Wilaya ya Mbinga kilichoketi Desemba 24, 2025.
.................................
 

Na Mwandishi Wetu, Mbinga 

KIKAO cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbinga kilichoketi  Desemba 24, 2025 chini ya Mwenyekiti wa chama hicho wa wilaya hiyo Joseph Mdaka kimempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  pamoja na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushindi wa kishindo walioupata katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. 

Aidha, kikao hicho kimempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Mhe. Jonas Mbunda na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga pamoja na madiwani wa Kata zote 48 za wilaya ya Mbinga kwa ushindi wa kishindo walioupata  katika uchaguzi huo.

Sambamba na pongezi hizo Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo imemtunuku cheti cha pongezi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makoli kwa kazi nzuri ya usimamizi wa Serikali pamoja na kuwa na mahusiano mazuri baina ya viongozi wa chama, serikali na wananchi.

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Joseph Mdaka alitumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Wilaya ya Mbinga kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika dhamana ya kuwaletea maendeleo na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa ili waweze kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/2030.

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Joseph Mdaka akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Makoli kutokana na utumishi wake uliotukuka.
Mbunge wa Mbinga Mjini, Jonas Mbunda akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.