Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi
.........................................................
Katika upepo wa kisiasa wa Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, historia mpya inaandikwa. Ni historia ya mshikamano, ya upendo, na ya siasa zenye sura ya matumaini. Ni historia inayowaweka kwenye ukurasa wa pekee Mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, na Mgombea mwenza wake, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi. Wamegawana majukumu si kwa vyeo, bali kwa dhamira ya kupeleka ujumbe wa matumaini na sera za maendeleo kwa kila kona ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Samia – Suluhu ya Matatizo, Mama wa Taifa
Katika mkutano uliofurika Morogoro Vijijini, maelfu ya wananchi walimiminika kumsikiliza Dk. Samia. Si kwa sababu ni Rais pekee mwanamke katika historia ya Tanzania, bali kwa sababu sauti yake imekuwa tiba ya changamoto zao. Alisimama na kuhesabu matunda ya uongozi wake: vituo vya afya kuongezeka kutoka vitano hadi 11, zahanati zikafikia 97, shule mpya zikajengwa, madarasa yakapanuliwa, na barabara zikabadilisha uso wa Morogoro kiuchumi.
Aliwaonesha wananchi kuwa CCM ni chama cha vitendo – kilichojenga maghala ya kuhifadhia mazao, kuleta mfumo wa Stakabadhi Ghalani, kugawa miche 80,000 ya tikiti maji bure, na kupeleka umeme vijiji 149 na vitongoji 417. Kwa lugha rahisi, Morogoro leo ni kioo cha Tanzania mpya – yenye afya bora, elimu imara, kilimo chenye tija na miundombinu ya kuunganisha wananchi.
“Tunapowasha taa vijijini, tunawasha ndoto za vijana wetu,” alisema Mama Samia, kauli iliyopigiwa makofi na vigelegele visivyoisha.
Nchimbi – Sauti ya Vijana, Mjumbe wa Uthubutu
Wakati Mama Samia akimimina matumaini Morogoro, Balozi Dk. Nchimbi alikuwa Mwanza – akihutubia wananchi wa Kwimba na Nyamagana. Alionekana kama kijana wa siasa aliyekomaa, kiongozi mwenye uthubutu na dira ya kizazi kipya.
Aliwakumbusha wananchi kazi kubwa iliyotekelezwa katika miaka minne na nusu ya Rais Samia: elimu bila malipo, barabara zilizojengwa, ajira kupitia viwanda, na huduma za afya zinazogusa maisha ya kila familia.
“Kwa kazi kubwa tuliyoifanya, zaidi ya wagombea wetu 91 wa udiwani Mwanza wamepita bila kupingwa,” alisema kwa kujiamini, huku maelfu wakishangilia kwa shangwe.
Kwa Nchimbi, CCM si chama cha maneno matupu. Ni chama kinachozaa matokeo. Ndiyo maana anatazamwa kama mwendelezo wa taswira ya mshikamano – kijana anayekuja na uthubutu mpya sambamba na Samia, Mama wa Taifa mwenye busara na ujasiri wa kuongoza nchi.
Bahati ya Agosti – Historia Inayoendelea Kuandikwa
Kwa Morogoro, mwezi Agosti ni kumbukumbu ya neema. Mwaka jana, Agosti, Rais Samia alizindua safari ya kwanza ya SGR – treni ya umeme iliyowaunganisha Watanzania kwa mwendo wa kasi. Mwaka huu, Agosti tena, amerudi Morogoro akiwa na ishara mpya – mgombea mwenza kijana, Dk. Nchimbi.
Bahati ya Agosti haijawa ya Samia peke yake, bali ni bahati ya wananchi. Bahati ya miundombinu, bahati ya kilimo, bahati ya elimu, na bahati ya mshikamano wa viongozi wa kizazi kipya.
Kampeni za Upendo, Si za Uchokozi
Kampeni za CCM mwaka huu zina upekee. Si za kejeli, si za chuki, bali ni kampeni za upendo na matumaini. Wananchi wanapewa takwimu zinazogusa maisha yao, wanaoneshwa miradi iliyotekelezwa na mipya inayoendelea. Hizi ni kampeni za maelezo yanayouzika bila kupigiwa debe – kwa sababu kila mwananchi anaona kwa macho yake yale yaliyofanywa na Serikali ya Mama Samia.
Hitimisho – Kura ni CCM, Suluhu ni Samia, Uthubutu ni Nchimbi
Kutoka Morogoro hadi Mwanza, upendo na matumaini vinamiminika kama mvua ya baraka. Samia na Nchimbi wamesimama kama jozi ya kihistoria – Mama wa Taifa na kijana wa uthubutu. Viongozi wawili waliogawana majukumu ya kupenya hadi kila kijiji na kila mtaa ili kusimulia ndoto ya Tanzania mpya.
Huu si wakati wa maneno matupu, bali wa kutenda. Si wakati wa hofu, bali wa matumaini. Kwa sauti moja wananchi wanatangaza:
Mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi akimndi mgombea
Mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi akimndi mgombea
Imeandaliwa na Victor Bariety – 0757 856 284
0 Comments